TANGAZO


Friday, May 4, 2012

Mtibwa yaipiga Azam 2-1, mchezo wa marudio, Simba yatwaa Ubingwa

 Wachezaji Vicent Barnabas (kushoto) wa Mtibwa, akichuana na Erasto Nyoni wa Azama FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo, ukiwa ni mchezo wa marudio baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Chamazi, unaomilikiwa na Azam, kumalizwa na mwamuzi wa mpambano huo kabla ya wakati wake, baada ya wachezaji wa Mtibwa kugomea Penanlti, iliyotolewa na mwamuzi wa mchezo huo, ambapo mwamuzi huyo, alimaliza mchezo zikiwa zimesalia dakika 2, kumalizika. Kamati ya Mashindano katika uamuzi wake iliamua mchezo huo kurudiwa leo, Uwanja wa Taifa na hivyo Mtibwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambapo sasa kwa matokeo hayo, Simba imetawazwa bingwa wa Ligi hiyo kwa mwaka 2012, kwani imefikisha ponti 59, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine za ligi hiyo. (PICHA ZOTE NA KASSIM MBAROUK)


 Mchezaji Shaaban Nditi wa Mtibwa, akiondoa mpira mbele ya Tchetche Kipre wa Azam FC, wakati wa mchezo huo.


 Mchezaji Juma Jaffari wa Mtibwa, akijaribu kumhadaa Aggrey Ambross wa Azam FC katika mchezo huo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini leo.


 John Bocco  wa Azam FC, kimtoka beki Salum Swed wa Mtibwa Sugar.


 Mchezaji Wazir Omar wa Azam FC, akimtoka Hussein Javu wa Mtibwa Sugar katika kipute hicho.


 Wachezaji wa Azam FC, wakilitia hekaheka lango la Mtibwa katika mchezo huo, uliokuwa wa vuta nikuvute.

Juma Jaffar wa Mtibwa Sugar, akiondoa mpira kwa kichwa huku akifuatwa na Tchetche Kipre (kushoto) wa Azam FC.


 Juma Jaffar wa Mtibwa Sugar, akimtoka Bolou Kipre wa Azam FC, wakati wa mchezo huo leo jioni, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.


 Juma Jaffar wa Mtibwa Sugar, akimwacha Bolou Kipre wa Azam FC, huku akitimua kuelekea kwenye lango la timu hiyo, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.


 Mashabiki wakifuatilia mchezo huo, kwenye jukwaa kuu la upande wa Magharibi mwa Uwanja huo.


 Tchetche Kipre wa Azam FC, akitafuta mbinu za kumtoka Juma Jaffari wa Mtibwa.


 Wachezaji wa Mtibwa Sugar, wakiswali ili kushangilia bao lao la pili dhidi ya Azam FC.


 Wachezaji wa Mtibwa Sugar, wakishangilia bao hilo, wakati wa mchezo huo leo jioni, Uwanja wa Taifa jijini dhidi ya Azam FC.

No comments:

Post a Comment