Waandishi na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mhariri wa michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa, wakilia kwa huzuni kubwa kutokana na msiba huo, wakati wakiingia kwenye viwanja vya Kanisa hilo kwa ajili ya kuuaga mwili wake, ambao baadaye ulisafirishwa hadi Goba, kwa ajili ya mazishi.
Msanii wa michezo ya kuigiza na ngonjera, Mrisho Mpoto 'Mjomba', akiwa amezungukwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya NHC, Ubungo, ambayo iko karibu na Kanisa la Anglikana, ulipoangwa mwili huo, wakitaka kusalimiana naye.
Wabunge Idd Azzan wa Kinondoni (kushoto) na John Mnyika wa Ubungo, wakiingia kwenye viwanja vya Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa.
Baadhi ya waandishi wa habari na wanamichezo, wakiwa nje ya Kanisa hilo, kwa ajili ya kusubiri kuuaga mwili wa marehemu, Rachel Mwiligwa.
Gari lililokuwa limeubeba mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa, aliyekuwa mhariri wa michezo wa gazeti la Mtanzania, likiungiza kwenye viwanja vya Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC, Dar es Salaam leo, kwa ajili ya Ibada ya kuuombea na kuuaga kwa mazishi yaliyofanyika baadaye, Goba nje kidogo ya jiji.
Jenenza lenye mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa, likishushwa kwenye gari na kuingizwa kwenye Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Ibada ya mwisho na kuagwa kabla ya kwenda kuzikwa maeneo ya Goba.
Mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Elizabeth Mjata, akiwa ameshikilia picha ya aliyekuwa mhariri wa michezo wa gazeti hilo, Rachel Mwiligwa, wakati jenenza lililokuwa limeubeba mwili wake likiingizwa kwenye Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC kwa Ibada ya mwisho na kuagwa leo.
Familia ya marehemu Rachel Mwiligwa, baba yake, Samwel, mama yake, Corona, mdogo wake, Lillian Mwiligwa pamoja na ndugu wengine wakiwa ndani ya Kanisa la Aglikana NHC, Ubungo, wakifuatilia Ibada ya mwisho ya kuuombea mwili wake kabla ya kuagwa kwa mazishi yaliyofanyika Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi, ndugu, jamaa na marafiki wakimwaga machozi ndani ya Kanisa hilo wakati mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa ukiagwa.
Familia ya marehemu Rachel Mwiligwa, ikiwa kanisani hapo, kwenye Ibada ya kumwombea na kumuaga kabla ya mazishi yake yaliofanyika Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo.
Dikoni Mkuu wa Kanisa la Aglikana, Ubungo NHC, akiendesha Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Rachel Mwilingwa, kabla ya kuagwa kwa ajili ya kwenda kuzikwa maeneo ya Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Waandishi, jamaa, ndugu na marafiki wa marehemu Rachel, wakiwa kwenye Ibada hiyo, kanisani hapo leo, mchana.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya (kushoto), akiwa pamoja na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari, Prince Bagenda (kulia) wakati wa ibada hiyo.
Mhariri wa gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia (kulia), akiwa pamoja na baadhi ya waandishi wa habari na wasanii wa muziki wa dansi kwenye ibada hiyo kanisani hapo leo.
Jenenza lililokuwa limewekwa mwili wa aliyekuwa Mhariri wa michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa, likwa limewekwa kanisani hapo, wakati wa Ibada ya kuuombea na kuuaga mwili wake.
Jamaa, marafiki na watu mbalimbali waliohudhuria kwenye Ibada ya kuuombea na kuuaga mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa, wakiwa katika Ibada hiyo, kanisani hapo.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), George John, akizungumza kwa niaba ya chama hicho kanisani hapo, wakati wa Ibada ya kuuombea na kuuaga mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mazishi ya marehemu Rachel Mwiligwa, Ajela Msangi, akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, kanisani hapo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari, Prince Bagenda, akizunguma kwa niaba ya kampuni yake hiyo, aliyokuwa akifanya kazi, marehemu Rachel Mwiligwa.
Mhariri wa gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia, ambalo Rachel Mwiligwa, alikuwa Mhariri wake wa Michezo, akielezea wasifu wa marehemu huyo pamoja na utendaji kazi wake.
Wabunge John Mnyika wa Ubungo na Idd Azzan wa Kinondoni, wakiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu Rachel mwiligwa kwenye Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC, baada ya Ibada ya kuuombea mwili wake.
Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, akiuaga mwili wa marehemu Rachel Mwiligwa pamoja na baadhi ya waandishi na jamaa za marehemu.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliokuwa bega kwa bega na marehemu Rachel Mwiligwa katika kuchapa kazi wakipita kuuaga mwili wake kanisani hapo leo mchana. |
Waandishi wa habari, wakilia kwa uchungu kutokana na kifo cha Mhariri huyo wa michezo, Rachel Mwiligwa. Hapa ni wakati walipokuwa wakiuaga mwili wake kanisani hapo.
Mwandishi wa habari za michezo, Mwani Nyangasa, aliyekuwa karibu sana na Mhariri wake huyo, marehemu Rachel Mwiligwa, akiwaongoza wenzake kumwaga chozi, wakati wa kuuaga mwili wake kwenye Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC, leo.
Kaka wa marehemu Rachel mwiligwa, wakiuaga mwili wa dada yao huyo, kanisani hapo leo mchana.
Baba wa marehemu Rachel Mwiligwa, Samwel Mwiligwa, akitokwa na machozi na kwikwi za kilio, wakati akiuaga mwili wa mtoto wake huyo, kanisani hapo.
Mama yake marehemu Rachel Mwiligwa, Corona, akiuaga mwili wa mtoto wake huyo.
Mdogo wa marehemu Rachel Mwiligwa, Lillian Mwiligwa akisaidiwa na ndugu pamoja na jamaa wakati akipita kuuaga mwili wa dada yake huyo kanisani hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wenzake, marehemu Rachel Mwiligwa, Charles Mateso (kushoto) na wenzake wakilibeba jenenza lake, wakati likitoka kanisani hapo kwa ajili ya kupelekwa maeneo ya Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa mazishi.
Picha ya marehemu Rachel Mwiligwa akiwa imeshikiliwa na mmoja wa jamaa yake wa karibu, wakati jenenza lake likitolewa kwenye Kanisa la Anglikana, Ubungo NHC kwa ajili ya kupelekwa makaburini Goba kwa mazishi.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nje ya kanisa hilo, wakati gari lililobeba jenenza lililoubeba mwili wa marehemu Rachel likielekea kwenye makaburi ya Goba kwa ajili ya mazishi.
Gari lililobeba jenenza lililoubeba mwili wa marehemu Rachel likielekea kwenye makaburi ya Goba kwa ajili ya mazishi, baada ya kumalizika shughuli za Ibada ya kuuombea na kuuaga mwili huo.
No comments:
Post a Comment