Wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa na mishipa ya fahamu (MOI), Muhimbili jijini Dar es Salaam, wakiwa wameshamtayarisha mgonjwa tayari kwa maonesho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), Viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
Gari la maonesho la Taasisi ya Mifupa na mishipa ya fahamu (MOI), Muhimbili jijini Dar es Salaam, likitoka kuelekea kwenye maonesho hayo.
Wafanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari na Meli (DOWUTA), Kitengo cha Makontena, wakipita kwa maandamano kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja, kwa ajili ya kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza, wakati wa maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari na Meli (DOWUTA), Kitengo cha Bandari ya Dar es Salaam, wakiwa kwenye maandamano hayo barabara ya Msimbazi, kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni, wakiwa kwenye maandamano hayo, mtaa wa Msimbazi kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), wakiwa kwenye maandamano hayo.
Wafanyakazi wa Chama cha Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU), tawi la Mofed, wakipita kwenye maandamano hayo kwenye mtaa wa Msimbazi kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini.
Wafanyakazi wa Chama cha Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU), Shirika la Ndege (Air Tanzania, wakipita kwa maandamano kwenye mtaa wa Msimbazi kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Kikundi cha Matarumbeta kikipita huku kikihamasisha wafanyakazi waliokuwa kwenye maandamano hayo, kuelekea Viwanjani hapo.
Wafanyakazi, wanachama wa Chama Cha Taasisi za Viwanda na Fedha (TUICO), kutoka wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), wakipita kwa maandamano hayo kwenye mtaa wa Msimbazi kuelekea viwanjani hapo.
Wafanyakazi, wanachama wa Chama cha Elimu ya Juu, Sayansi na Afya (TAGHE), kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi jijini, wakiwa kwenye maandamano hao, kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), leo.
Wafanyakazi, wanachama wa Chama Cha Taasisi za Viwanda na Fedha (TUICO), kutoka Kampuni ya Azam, wakipita kwa maandamano hayo kwenye mtaa wa Msimbazi kuelekea viwanjani hapo.
Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), Bohari ya Jiji, wakipita mbele ya mgeni rasim wa maadhimisho hayo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza.
Walimu kutoka Manispaa za Dar es Salaam, kupitia Chama cha Walimu Tanzania (CWT), wakipita mbele ya mgeni rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza.
Maandamano ya magari yakipita barabara ya Morogoro kuelekea Viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho hayo.
Magari yenye bidhaa na vifaa mbalimbali vya kazi yakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi 'Mei Dei' jijini leo.
Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali wakiwa katika wimbo wao wa mshikamano mara baada ya kupokelewa maandamano yao na mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza, akiwahutubia wafanyakazi wa Sekta mbalimbali, baada ya kuyapokea maandamano yao katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani 'Mei Dei', Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini leo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza, akimkabidhi cheti na hundi, mfanyakazi bora wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Humphrey Bwogi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza, akimkabidhi cheti na hundi ya Sh. 500,000, mfanyakazi bora wa Elimu ya Msingi, Kinondoni, Hyacintha Madinda.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantumu Mahiza, akimkabidhi cheti na hundi ya Sh. 1,000,000, mfanyakazi bora wa Bandari, Hawa Kapteni.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni, upande wa Elimu ya Msingi, wakiwa katika picha ya pamoja na mfanyakazi bora, Hyacintha Madinda (aliyeshikilia cheti), mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mahakama, wakifuatilia matukio mablimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye maadhimisho hayo, viwanjani hapo.
Wasanii wa bendi ya Magereza 'Wana - Mkote Ngoma ', wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo, viwanjani hapo.






















.jpg)





No comments:
Post a Comment