Wakili wa wajane wa Osama Bin Laden na mabinti zake amesema, familia hiyo imepewa kifungo cha siku 45 kila mmoja kwa kuishi nchini Pakistan bila kibali. Wakili huyo, Atif Ali Khan ameambia BBC wanawake hao wametumikia vifungo vyao na wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani kwao katika majuma mawili yajayo.
Wajane wawili ni raia wa Saudi arabia huku mwenzao wa tatu akiwa mzaliwa wa yemen. Bw Khan amesema wameshauriana na serikali ya Saudi Arabia kuwakubalia wajane wawili kurejea nyumbani huku mjane anayetoka Yemen akikubaliwa kurudi nyumbani.Wajane watatu walichukuliwa na maafisa wa usalama baada ya Osama Bin Laden kuuawa katika operesheni ya kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan hapo mwezi Mei.
No comments:
Post a Comment