TANGAZO


Friday, April 27, 2012

Viongozi wa Ecowas kutuma majeshi


Mkutano wa Ecowas
Jumuia ya Ecowas
Viongozi wa Mataifa ya Afrika ya magharibi wameafikiana juu ya kutuma vikosi huko Mali na Guinea Bissau kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo.
Shirikisho la Kikanda Ecowas liemesema baada ya mkutano wa dharura wa viongozi kua wanatarajia kua nchi hizo mbili zitaandaa uchaguzi wa Rais katika kipindi kizichozidi miezi 12.
Jeshi la Guinea Bissau
Jeshi la Guinea Bissau
Ecowas litatuma kati ya vikosi 500 na 600 haraka iwezekanavyo nchini Guinea Bissau.
Takriban askari 3000 kutoka kanda hio wako tayari kutumwa nchini Mali kuunga mkono serikali ya mpito ili kukabiliana na waasi wanaodhibiti eneo la kaskazini la nchi.
Mwandishi wa BBC kwenye mkutano wa mjini Abidjan, John James anasema kua hakuna mda kamili uliowekwa wa kutuma vikosi nchini Mali, kwa sababu viongozi wanasubiri wakuu wa Mali wawatumie maelezo ya ushirikiano wao katika mpango huo.
Haijafahamika bado ni nchi zipi za eneo hilo zilizotuma vikosi katika kikosi cha Ecowas,hata kikiwa tayari, kuna haja ya fedha na vifaa kutoka nje kabla ya mchango huo kutumika.
Hata hivyo viongozi wa Ecowas wameonya kua endapo wakuu wa Guinea-Bissau watakaidi uwamuzi wa kutuma vikosi vya Ecowas katika kipindi cha saa 72, watakabiliwa na vikwazo.

No comments:

Post a Comment