Wapiganaji wa Taliban wameshambulia gereza kaskazini magharibi mwa Pakistan, na kuwaachilia huru wafungwa karibu 400.
Polisi wanasema washambuliaji walitumia bunduki na maguruneti katika shambulio hilo jana usiku huko Bannu, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Wakuu wanasema kati ya wafungwa waliotoroka ni wapiganaji na wahalifu wakubwa.
Mmoja wao, Adnan Rasheed, alihukumiwa kifo kwa kupanga njama ya kumuuwa rais wa zamani wa Pakistan, Pervez Musharraf.
No comments:
Post a Comment