TANGAZO


Friday, April 20, 2012

Sporting, Atletico za shinda


Timu ya Sporting Lisbon ilijiweka katika nafasi nzuri ya kufaulu kwa fainal ya kombe la Euro baada ya kuichapa Athletico Bilbao 2-1
Athletico Bilbao washerehekea bao lao
Bilbalo ndio waliokuwa wakwanza kufunga kabla ya Sporting kufunga magoli mawili ya haraka haraka.
Ushindi huo wa Sporting ulishangaza kwani walionekana kupoteza matumaini kwani vijana wa Bilbao kutoka Uhispania walikuwa wakitawala mechi hiyo na kukosa mabao mengi.

Athletico Madrid 4-2 Valencia

Kwengineko Atletico Madrid iliibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Valencia katika mechi iliyojumuisha timu za Uhispania.
Mechi hiyo ya nusu fainali ilikuwa na msisimko kutokana na kwamba katika ligi ya nyumbani Valencia wako juu ya Athletico baada ya kuwafunga 1-0 katika duru yakwanza ya ligi ya Uhispania.
Athlerico ndio iliyokuwa ya Kwanza kufunga kupitia Radamel Falcao kabla ya Velencia kukomboa.
Hata hivyo Velencia ilijipatia mabao yake mawili kutokana na ulegevu wa dakika za mwisho wa timu ya Athletico Madrid.
Timu zote nne zitakutana tena wiki ijayo katika duru ya pili ya michuano ya nusu fainali.

No comments:

Post a Comment