Makamu wa Rais, Dk. Mohammed
Gharib Bilal, akimfariji Mama mzazi wa msanii wa Filam, marehemu Steven
Kanumba, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya
Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Aprili 10, 2012.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed
Gharib Bilal, akiondoka kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni baada ya
kuuaga mwili wa marehemu Steven Kanumba , jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, Aprili 10, 2012.
Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kanumba viwanjani hapo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangala na Waziri wa Nyumba, Ardhi na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kanumba.
Mtoto wa Mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela, Willium Malecela, akitoa heshima za mwisho kwa mwili huo, viwanjani hapo.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Ujerumani (Dueche Welle), Aboubakary Liongo, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kanumba.
Mama wa msanii wa maigizo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mutegoa, akiushika mwili wa mwanawe huyo, wakati wa kuuaga katika Viwanja wa Leaders Club, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia), akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ridhwan Kikwete (katikati) pamoja na Mbunge wa Kinodoni, Idd Azzan, wakati wa kuuanga mwili wa msanii Steven Kanumba, Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamekaa kusubiri zamu zao za kuuaga mwili wa marehemu Kanumba kwenye viwanja hivyo leo asubuhi.
Baadhi ya ndugu wa familia ya msanii wa maigizo, marehemu Steven Kanumba, wakiwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuuaga mwili wake.
Mhudumu wa huduma ya mwanzo kutoka Msalaba mwekundu (kulia), akitoa msaada wa huduma kwa ndugu wa jama anayemsaidia kubeba.
Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora (kulia), akiwa na bintiye, wakati wa kuuaga mwili wa mwanawe, Steven Kanumba, kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ridhwan Kikwete (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba, wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Kanumba, viwanjani hapo.
Waibaji wa kwaya ya Shallom, wakitoa burudani wakati wa kuuaga mwili huo.
Msanii wa vichekesho na mtangazaji wa TBC, Bi Kiroboto, akiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali ya kuuaga mwili huo.
Wasamaria wema wakisaidia kumbeba muombolezaji aliyedondoka wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Kanumba, viwanjani hapo.
Baadhi ya wasanii mbalimbali wakiwa wamekaa karibu na jenenza lililokuwa na mwili wa msanii mwenzao, marehemu Steven Kanumba.
Baadhi ya watangazaji wa Radio Uhuru, wakiwa kwenye viwanja vya Leaders Club, wakati wa hafla ya kuuaga mwili huo.
Umati wa waombolezaji ukijitahidi kujongea karibu ili kuweza kuliona jenenza na kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba, huku wakizuiwa na askari wasisogee kutokana na kuwa na msongamano wa watu katika eneo hilo.
Vijana wakiwa wamejipanga kandokando ya barabara kwa ajili ya kuulaki mwili wa marehemu Steven Kanumba.
Umati wa waombolezaji ukielekea kwenye makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya kwenda kuuzika mwili wa marehemu huyo.
Foleni za magari zikend sambamba na waombolezaji waliokuwa wakielekea kwenye makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya kwenda kuuzika mwili wa maremu Steven Kanumba.
Umati wa waombolezaji ukiwa umefunga na kufunika viwanja vya Leaders Club, hukun baadhi yao wakiwa wameshaanza kuelekea kwenye makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya kuuzika mwili wa marehemu huyo.
Kijana akiwa amebebwa kwenye machela baada ya kudondoka na kisha kuzimia wakati wa shughuli za kuuaga mwili kwenye viwanja vya Leaders Club leo.
Mwakilishi wa wasanii wa maigizo JB, akizungumza katika hafla ya kuuaga mwili, viwanja vya Leaders Club.
Baadhi ya waandishi na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa kazini wakati wa kuuaga mwili huo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika hafla ya kuuaga mwili huo, ambapo alitangaza Serikali kutoa ubani wa sh. milioni 10 kwa ajili ya msiba huo.Kulia ni Mc wa hafla hiyo, Taji Liundi
Kijana mwombolezaji, akimchupishwa ukuta wa makaburi ya Kinondoni, msichana ili kuweza kuingia kwenye makaburi hayo, kujionea shughuli za mazishi ya msanii wa maigizo, aliyefariki, marehemu Steven Kanumba, Dar es Salaam
Askari Polisi wa kikosi cha farasi, akizunguka mitaani maeneo ya makaburi ya Kinondoni kuangalia usalama katika eneo la mazishi ya msanii huyo.
Waombolezaji wakiwa ndani ya makaburi ya Kinondoni huku askari Polisi wakichunga usalama katika eneo hilo, huku shughuli za mazishi zikiendelea makaburini hapo.
Vijana waombolezaji wakiwa wamekaa kusubiri shuguli za mazishi zianze, bila kujua kwamba shughuli hizo zilikuwa zikiendelea kwenye makaburi hayo.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), wakiangalia usalama kwenye makaburi hayo.
Askari akipita na mbwa wake mbele ya waombolezaji waliokuwa wamekaa chini kwenye makaburi hayo huku shughuli za mazishi zikiedelea.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wametulia chini kusubiri shughuli za mazishi ya mwili wa marehemu Steven Kanumba.
Jenenza lililoubeba mwili wa msanii wa maigizo, marehemu Steven Kanumba, likishushwa kwenye kaburi, wakati wa mazishi yake, yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Jenenza lililokuwa na mwili wa marehemu Steven Kanumba likishushwa kwenye kaburi.
Askofu akiuombe mwili wa marehemu Kanumba, mara baada ya jenenza lenye mwili wake kushushwa kaburini wakati wa mazishi hayo.
Vijana waombolezaji wakiwa wamepanda juu ya mti kwenye makaburi hayo, ili kushuhudia shughuli hizo zilivyokuwa zikiendelea.
Baadhi ya ndugu wa familia ya marehemu Steven Kanumba wakiwa kwenye makaburi ya Kinondoni wakati wa shughuli za mazishi ya marehemu huyo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik (kulia) na mwakilishi wa familia ya marehemu Kanumba, John Shibuda, wakiwa kwenye makaburi ya Kinondoni wakati wa mazishi ya marehemu huyo, leo jijini.
Mwakilishi wa wazee wa marehemu Kanumba, John Shibuda, akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Kanumba kwa niaba ya familia hiyo.
No comments:
Post a Comment