TANGAZO


Monday, April 16, 2012

Rais Dk. Shein Ziarani Pemba, kukagua maendeleo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea katika uwanja wa ndege wa Karume, Pemba, leo wakti alipowasili kisiwani humo kwa ziara maalumya kuangalia maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii. (Picha na Ramadhan Othman, Pemba)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na  wananchi waliojitokeza kumpokea Uwanja wa ndege wa Karume Pemba alipowasili kisiwani humo kwa ziara maalum ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za kijamii.


Afisa Tawala, Juma Shaaban wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, akitoa taarifa ya Mkoa kwa viongozi, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa katika ziara maalum ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali mkoani humo katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba.

Baadhi ya Viongozi na watendaji walioshiriki katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Sheib, wakimsikiliza Rais, alipokuwa akizungumza na watendaji hao, wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Mkoa wa Kasakazini Pemba, katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo.


Wanachama wa Muwape Saccos ya Mtemani Wete Pemba, wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wanachama wa Saccos hiyo wakati wa uzinduzi rasmi leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wanachama wa Muwape Saccos ya Mtemani Wete Pemba, wakati akiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Kijamii Mkoani humo. Pia Rais alizindua Saccos hiyo leo. Kulia ni Rashid Said, Katibu wa Saccos na katikati ni Salim Khamis Mwenyekiti wa Saccos hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na mtoto Suleiman Shaaban Juma pamoja na wanachama wa Kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa, wakati alipofika kuzindua mradi wa uzalishaji sabuni kwa kutumia mashine maalum ya Mkipi Miliki, leo Aprili 16, 2012, kisiwani Pemba.  


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa, ambayo inazalisha sabuni kwa kutumia mashine maalum, alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizindua  Kampuni ya Mkipi Miliki, Tungamaa ambayo inazalisha sabuni kwa kutumia
mashine maalum, alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia Sabuni iliyotengenezwa katika kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa, ambayo hutumia mashine maalum, katika uzalishaji wa bidhaa hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu, George Buchwafwe.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu George Buchwafwe, wakati alipokuwa akiangalia Sabuni iliyotengenezwa katika kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa, wakati wa ziara hiyo, mkoani humo leo.

No comments:

Post a Comment