TANGAZO


Saturday, April 28, 2012

Ombi la Sudan Kusini lajadiliwa Arusha

Viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki wamemaliza kukutana mjini Arusha, ambapo ombi la Sudan Kusini kuwa mwanachama wa jumuia hiyo limejadiliwa.

Nembo ya Jumuia ya Afrika Mashariki
Mkutano umeamua kuunda jopo litalokwenda Sudan Kusini kutathmini ikiwa nchi hiyo inatimiza vile vipengee vinavofaa kabla ya kukubaliwa kuwa mwanachama.
Jamhuri Mwavyombo, aliyehudhuria mkutano anasema, linalotia wasiwasi ni kama Sudan Kusini inafaa kukubaliwa kwenye jumuia wakati iko vitani na Sudan.
Anasema kuna maoni tofauti - kuna wale wanaofikiri Sudan Kusini inaweza kusaidiwa kumaliza mgogoro wake na Sudan endapo imo ndani ya jumuia.
Wengine wanaona afadhali kusubiri hadi vita vitulie.
Lakini kwa sasa ombi la Sudan Kusini linaangaliwa kwa makini, anasema mwandishi wetu.
Sudan iliwahi kuomba kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki lakini ilikataliwa.

No comments:

Post a Comment