Ripoti kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo
zinasema kuwa mapigano makali yametokea baina ya jeshi la serikali na askari
watiifu kwa jenerali aliyeasi, Bosco Ntaganda.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema, mvutano unaozidi mashariki mwa Congo ndio tatizo kubwa kabisa linalokabili baraza jipya la mawaziri, ambalo lilitangazwa jana.
Jenerali Ntaganda ni mpiganaji wa zamani, ambaye anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuwaajiri watoto kwenye jeshi lake.
Piya anasakwa na wakuu wa Congo.

No comments:
Post a Comment