TANGAZO


Monday, April 23, 2012

Marriner kuchezesha pambano Manchester

Andre Marriner ametajwa atakuwa mwamuzi wa pambano la kukata na shoka kati ya Manchester City na Manchester United tarehe 30 mwezi huu wa Aprili.

Andre Marriner kuchezesha mtanange wa Manchester
Andre Marriner kuchezesha mtanange wa Manchester

Marriner, mwenye umri wa miaka 41, alichezesha mechi kati ya Manchester United na Liverpool mwezi wa Oktoba mwaka jana, ambapo timu hizo zilitoka sare na mtanange huo utakumbukwa ulipozua balaa la maneno ya kibaguzi ambayo Patrice Evra alirushiwa na Luis Suarez.
Manchester City inawanyatia mahasimu wao hao kwa karibu wakiwa nyuma kwa pointi tatu tu lakini wana hazina kubwa ya mabao ya kufunga.
Marriner, anayetokea Sheldon West Midlands, ameshachezesha mechi tatu za Manchester United msimu huu dhidi ya Norwich, Liverpool na Bolton- lakini hajachezesha mechi ya Manchester City.
Mechi yake ya mwisho aliyochezesha kukutanisha timu zinazotoka mji mmoja wa Manchester ilikuwa mwezi wa Februari mwaka 2011 wakati Wayne Rooney alipofunga bao la ushindi kwa tikitaka kwenye uwanja wa Old Trafford. Manchester United walishinda kwa mabao 2-1.
Meneja wa Manchester United Sie Alex Ferguson alimshutumu sana Marriner baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na Liverpool katika uwanja wa Anfield mwezi wa Septemba mwaka 2009, akidai alikuwa akitoa uamuzi kwa woga kutokana na makelele ya washangiliaji.
Marriner msimu huu amekwishatoa kadi tano nyekundu, ikiwemo ya David Dunn wa Blackburn walipocheza dhidi ya Wigan mwezi wa Novemba ambapo alikubali bao baada ya Morten Gamst Pedersen kujipasia mwenyewe mpira wa kona.
Manchester City wanaweza kukamata usukani wa Ligi zikiwa zimesalia mechi mbili kabla msimu kumalizika iwapo watailaza Manchester United katika uwanja wa Etihad.
Wameweza kurejea katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi mwishoni mwa wiki baada ya kuilaza Wolves 2-0, wakati Manchester United walivutwa shati walipolazimishwa sare ya mabao 4-4 na Everton.

No comments:

Post a Comment