TANGAZO


Friday, April 20, 2012

Maelfu waandamana Misri

maelfu wamepiga kambi Tahrir
Maelfu yaraia wa Misri wameandamana katika medani ya Tahir mjini Cairo kushinikiza watalawa wa kijeshi kuyakabidhi madaraka kwa raia.Maandamano ya leo yametajwa kuwa makubwa zaidi katika miezi ya karibuni.
Maandano ya leo yalihusisha mirengo yote ya kisiasa nchini Misri, ikiwemo mirengo ya kiisilamu, walio na msimamo wa kati na kupinga sera za dini, mrengo wa kushoto na vijana walioshinikiza mapinduzi. Hata hivyo makundi yote na malengo tofauti.
Mrengo wa kiisilamu unatuma ujumbe kwa watawala wa kijeshi kulalamikia kufutwa kwa wagombea wake wa urais. Mrengo usiyofuata sera za dini unataka makundi ya kiisilamu kutokubaliwa ushawishi katika baraza kuu la kuunda katiba.
Vugu vugu la vijana wanamageuzi nao wanapinga kuendelea na utawala wa kijeshi wakati nchi hiyo ikijiandaa kuandika katiba mpya. Kuna maandamano mengine yapo kiasi tu katika miji mingine ya Alexandria na Suez.
Kila kundi limeweka kambi yake ndani ya medani ya Tahrir, na kinachosikika ni kelele za kulaani watawala wa jeshi, huku milolongo ya raia ikiendelea kuingia medani hiyo.

No comments:

Post a Comment