Bosco Ntaganda
Mamia ya wanajeshi wameasi jeshi
la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Duru za kibalozi zimesema
wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa kiongozi wa waasi Bosco Ntaganda
walianza kuondoka jeshini mapema wiki hii.
Ntaganda anatakiwa na mahakama ya kimataifa- ICC
kwa kutekeleza dhuluma za vita.Wasi wasi umetanda mjini Goma Mashariki
mwa DRC ambapo ni ngome kuu ya Ntaganda.Wiki jana Ubeljiji ilitaka serikali ya Congo kumkamata Bosco Ntaganda na kumkabidhi kwa ICC. Kamanda huyo wa jeshi ameshtakiwa kwa kuwasajili watoto jeshini, mauaji na ubakaji.
Katika ziara yake mjini Kinshasa, Waziri wa Mambo ya nje wa Ubeljiji Didier Reynders alimuelezea rais Joseph Kabila kwamba sifa ya serikali yake inapata doa kwa kushindwa kumkabidhi Bosco Ntaganda kwa ICC.
Mhariri wa BBC wa masuala ya Afrika Martin Plaut amesema hatua ya majeshi tiifu kwa Ntaganda kuasi jeshi la taifa ni onyo kuwa watajibu jaribio lolote kumkamata kamanda wao Bosco Ntaganda.

No comments:
Post a Comment