TANGAZO


Sunday, April 1, 2012

Jeshi la Mali laahidi kuacha uongozi

Viongozi wa mapinduzi ya Mali wamesema kutoka Jumapili, watarejesha katiba ya zamani pamoja na taasisi za taifa.
Amadou Sanogo
Wanajeshi hao katika mji mku, Bamako, wamepewa muda hadi Jumapili usiku kuanza kukabidhi madaraka kwa raia; ama sivyo, watakabili vikwazo vya kiuchumi kutoka nchi jirani.
Kiongozi wa mapinduzi, Kepteni Amadou Sanogo, alisema hayo wakati kuna ripoti kuwa wanajeshi wa serikali wameukimbia mji wa kaskazini wa Timbuktu, baada ya kusikia kuwa wapiganaji wa kabila la Tuareg wanaujongelea mji.
Timbuktu imezingirwa na wapiganaji wa Tuareg na ndio mji wa mwisho uliokuwa chini ya mamlaka ya jeshi kaskazini mwa Mali.
Sasa unalindwa na wanamgambo wa Kiarabu wa mji huo.
Jumamosi wapiganaji waliuteka mji wa Gao wenye ngome ya jeshi, na hivo kuzidisha mafanikio yao kaskazini.

No comments:

Post a Comment