Kaimu kocha wa Chelsea Di Matteo akielekeza jambo
Kaimu kocha wa Chelsea,Roberto
Di Matteo anaamini klabu hiyo bado ina sifa ya kuwa klabu muhimu katika
nyanja ya kimataifa licha ya kutowahi kamwe kunyakua kombe la ligi ya
mabingwa wa Ulaya.
Ametoa kauli yake hiyo wakati Chelsea
inajitayarisha na mkondo wa pili wa mechi ya robo fainali na Benfica ya
Ureno. Chelsea ilishinda mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa bila.Wakiepuka kushindwa na Benfica siku ya Jumatano,watafaulu kuingia nusu fainali kwa mara ya sita katika misimu tisa ambapo watapambana na Barcelona.
"Mkiangalia muongo uliopita wa klabu hii,utaona imekuwa muhimu kitaifa na kimataifa.," alisema.
Kiungo Ramires nae pia alitamka kuwa klabu hiyo inaheshimiwa sana nchini kwao Brazil kama namna vilabu vya Barcelona au Real Madrid vinavyoheshimiwa.
No comments:
Post a Comment