TANGAZO


Saturday, March 10, 2012

wauguzi wanawake wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),Yatoa msaada wodi ya watoto

Wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakiwa na zawadi mbalimbali ambazo waliziandaa kuwapatia akina mama wanaouguza watoto wao katika Taasisi hiyo. Wanawake hao ambao walichangishana kwa ajili ya kuwagawiwa wagonjwa, walifanya hivyo leo ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Wakielekea wodi ya watoto kugawa msaada huo
Meneja Uhusiano Msaidizi wa MOI, akizungumza na baadhi ya akina mama wanaouguza watoto kabla ya kuwagawia msaada
Mmoja wa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Mtoto huyo anasubiri kufanyiwa upasuaji wa uvimbe huo alionao mgongoni
Wakiwa tayari kuanza kugawa msaada
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya MOI, akizungumza kabla ya kuanza kugawa
Wakimwangalia mmoja wa watoto walio chumba cha watu mahututi
Wakiwapatia msaada akina mama wanaowauguza watoto wao
Mmoja wa manesi hao akigawa  awadi kwa mmoja wa wagonjwa hao

No comments:

Post a Comment