Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish na nahodha wake Steven Gerrard wametoa wito kwa kikosi chao kumaliza hali ya kuteleza iliyojitokeza hivi karibuni na kushinda pambano dhidi ya majirani wao Everton siku ya Jumanne.
Liverpool wamepoteza mechi zao tatu zilizopita, ikiwa ni hali mbaya kuwatokea tangu mwaka 2003, na Dalglish amesisitiza kila mmoja katika klabu hiyo anapaswa kuwajibika.
Alisema: "Kila mmoja anahitajika kusimama kidete na kuwajibika na tutaona kile tutakachokifanya."
Gerrard kwa upande wake ameongeza: "Tunahitaji kubadilika na ili tuoneshe tumebadilika ni lazima kushinda dhidi ya Everton."
Liverpool haijaonja ushindi katika mechi za ligi tangu tarehe 31 mwezi wa Januari, ingawa iliichapa Cardiff kwa mikwaju ya penalti na kufanikiwa kunyakua Kombe la Carling mwezi wa Februari.
"Inategemea na timu unazokabiliana nazo, lakini kusema ukweli si rekodi nzuri unayotazamia kutoka kwa Liverpool," alisema Dalglish.
"Hatutaki kuzoea tabia ya kupoteza michezo, lakini kati-kati ya kupoteza mechi tulifanikiwa kushinda Kombe la Carling.
Iwapo Everton itafanikiwa kuilaza Liverpool katika uwanja wa Anfield basi Everton wataichukua nafasi ya saba inayoikalia sasa.
Na Gerrard anawataka wachezaji wenzake kusaidia wanavyoweza wasipoteze tena mchezo.
"Wachezaji wanatakiwa kubeba jukumu kutokana na sehemu tuliyopo hivi sasa kwenye msimamo wa ligi," alisema.
"Haipendezi kwa klabu kama yetu kuwa mahali tulipo. Hatuna buti kutafuta jawabu la kuimarika.
Liverpool wakimaliza mtanange na majirani wao wa Everton, watakabiliana na Stoke katika robo fainali ya kuwania Kombe la FA siku ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment