Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na viongozi kadhaa wa Mataifa ya Kiarabu wamewasili nchini Iraq kwa mkutano wa kilele wa Jumuia ya nchi za Kiarabu.
Kama anavyoarifu mwandishi wetu Wyre Davies kutoka mji mkuu wa Iraq, Baghdad, kuwepo kwao huko kunafaa kuizidishie Syria shinikizo ili kukomesha ghasia.
Lakini kukosa kuhudhuria kwa viongozi kadhaa kutoka Mataifa ya Ghuba kunaweza kutoa sura ya mgawanyiko juu ya jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo.
Umoja wa Mataifa unakadiria kua zaidi ya watu 9,000 wameuawa nchini Syria katika kipindi cha mwaka mmoja wa ghasia na kumekuwepo miito kutoka katika Mataifa ya Kiarabu yakitaka hatua za moja kwa moja dhidi ya serikali ya nchi hio.
Viongozi wengine wakiwemo wa nchi jirani na Syria, kama Lebanon na Iraq wana wasiwasi juu ya nini kitafuata ikiwa utawala wa Bashar al Assad utapinduliwa. Kwa hio wameomba tahadhari ifanywe na kusema kua pasiwepo uingiliaji wa Mataifa ya kigeni nchini Syria.
Wasiwasi umetanda katika eneo zima. Iraq ndio bado inajikwamua kutoka muongo mzima wa mgogoro kukiwa na hali ya tahadhari mjini Bagdad.
Wakati Mkutano wa viongozi wa Kiarabu ukianza majira ya adhuhuri zilitoka taarifa za milipuko miwili karibu na eneo moja la mji linalojulikana kama la kimataifa ambalo haliko mbali na majengo ambako Mkutano unaffanyika.
No comments:
Post a Comment