TANGAZO


Wednesday, March 14, 2012

Tevez kushiriki dhidi ya Chelsea


Klabu ya Manchester City huenda isimtumie mcheza kiungo wake Gareth Barry kwa mchuano wa kesho wa Ligi ya Europa dhidi ya Sporting Lisbon kwenye uwanja wao wa Etihad.
Carlos Teves
Carlos Teves

Mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya England anakumbwa na maumivu ya mgongo na Meneja wake Roberto Mancini huenda akampuzisha kwa mchuano huo muhimu.
Barry anajiunga kwenye orodha ndefu ya majeruhi Vincent Kompany na Pablo Zabaleta, pia Joleon Lescott (kiwiko) ingawa inasemekana huyu amepata nafuu.
Mshambuliaji Carlos Tevez hakuorodheshwa kushiriki michuano ya Ulaya na hivyo hawezi kusaidia.
Meneja Roberto Mancini anasema hata hivyo kua Carlos Tevez anaweza kushiriki mchuano dhidi ya Chelsea wiki ijayo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, hajashiriki michuano yoyote kwa kipindi kirefu tangu ashutumiwe kwa kukataa kupasha viungo joto wakati wa pambano la Ligi ya mabingwa klabu yake ilipofungwa na Bayern Munich mwezi Sebtemba mwaka jana.
Tangu hapo alirejea baada ya kuomba msamaha na kushriki mashindano ya wachezaji wa akiba ili kufikia viwango vya kucheza michuano ya kiwango cha mashindano makubwa.
City itachuana na Chelsea siku ya jumatano tarehe 21 Machi wakati ambapo huenda ikawa nyuma ya Manchester United kwa pointi 4.
United inachuana na Wolves ugenini jumapili huku mchuano wa City unaofuata ni dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa nyumbani wa Etihad.
Tevez alifunga mabao 44 katika mechi 69 za Ligi kuu ya Premier katika msimu wake wa kwanza hadi mgongano wa mwezi Septemba.
Alikaribia kuihama klabu hio katika dirisha la usajili la mwezi januari baada ya kusafiri kwenda Argentina bila ruhusa ya klabu yake, lakini sasa anaonekana ataiwakilisha klabu yake katika michuano ya kushindani Kombe la Ligi kuu.
City ni ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu ya England baada ya kupoteza mechi yake dhidi ya Swansea siku ya jumamosi iliyopita ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hio kukosa kuongoza msimamo wa Ligi katika kipindi cha miezi mitano.

No comments:

Post a Comment