
Mchezaji
wa Simba, Felix Sunzu, akimkabidhi jezi yake, mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Televisheni ya klabu ya Simba, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa (wa pili kushoto), aliyopewa katika hafla ya
uzinduzi wa TV hiyo, ambayo itaanza kwa kurusha
vipindi vya mambo mbalimbali yanayohusu klabu hiyo na baadaye kuanza
kurusha vipindi vyake masaa 24. Hafla hiyo, ilifanyika jana usiku, Quality
Center, jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwanachama timu hiyo, Profesa Juma Kapuya, kulia ni Makamu Mwenyekiti
wa klabu hiyo, Geofrey Nyange Kaburu na Mwenyekiti wa klabu Ismail Aden Rage. (Picha na Mpiga picha wetu)

Mchezaji
wa zamani wa klabu ya Simba, Zamoyoni Mogella, akizungumza katika
uzinduzi huo, ambapo aliwaasa wachezaji wa timu hiyo, kuonyesha uwezo wao
wote hasa katika mchezo wa kesho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda. Kulia ni Msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kwamwanga.

Mgeni
rasmi, Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa, akimlisha keki, Mwenyekiti
wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage wakati wa hafla hiyo. Kutoka kushoto ni
Makamu wa pili wa TFF, Ramadhan Nassib, Profesa Juma Kapuya na
kulia ni Mzee Kinesi.

Mgeni
rasmi Naibu, Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa akikata keki kuashiria
uzinduzi rasmi wa televisheni hiyo. Kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa
TFF, Ramadhan Nassib, Profesa Juma Kapuya, Mzee Kinesi (kulia) na
Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro, George Kavishe.

Mgeni
rasmi Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe cha kompyuta tayari kwa kuwasha kipindi cha Televisheni kinachoonyesha
matukio mbalimbali ya klabu ya Simba. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
Simba Geofrey Nyange Kaburu, Mwanachama wa Simba, Profesa Juma Kapuya
na kutoka kushoto ni Msemaji hiyo, Ezekiel Kamwanga na Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage.

Wanaofungua shampeni, kutoka kulia ni Charles Hamka, Said Tuli na Swedi Mkwabi.

Shabiki
mkubwa wa Yanga, Motisha naye, alihudhuria katika sherehe hiyo, hapa
akitambulishwa huku mwalimu wa makipa wa Simba, James Kisaka, akimuwekea jezi
ya Simba.

Mchezaji wa timu ya Simba, Said Nasoro Cholo, akitambulishwa katika hafla hiyo.

Wazee
wa Friends of Simba, wakibadilishana mawazo kutoka kulia ni Evance
Aveva, Nick Magarinza, Juma Pinto, Salim Try Again, na Redemptus Masanja
wa NBC.

Mashabiki na wadau mbalimbali wa Simba wakiwa katika hafla hiyo.

Waandishi wa habari kutoka kulia, Dina Ismail, Jesca Charles, na Asha Kigundula wakiwa katika hafla hiyo.

Kutoka kulia ni Jerry, Bawazir, Musley na Hassan Hasanoo wa Friends of Simba.

Wachezaji wa timu ya Simba wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba, wakiwa katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment