TANGAZO


Monday, March 12, 2012

Rosicky kuendelea kuichezea Arsenal

 
Tomas Rosicky
Rosicky amewaridhisha mashabiki wa Arsenal katika mechi za hivi majuzi

Kiungo cha kati wa klabu ya soka ya Arsenal, Tomas Rosicky, ambaye pia ni maarufu katika kushambulia, ametia saini mkataba mpya na klabu hiyo.
Rosicky yumo katika hali nzuri sana msimu huu, na ameweza kuifungia Arsenal mara mbili katika mechi tatu zilizopita.
Meneja Arsene Wenger amesema: "Siku zote nimevutiwa sana na anavyocheza Tomas na hasa uwezo wake mkubwa, na nimefurahi sana ameamua kuendelea kuichezea klabu".
Rosicky, mwenye umri wa miaka 31, na ambaye ni nahodha wa timu ya Jamhuri ya Czech, alijiunga na The Gunners mwaka 2006, wakati huo akitoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Bado haijafahamika mkataba huo mpya ni wa muda gani.

No comments:

Post a Comment