TANGAZO


Thursday, March 15, 2012

Rais Karzai asema NATO iondowe askari

Rais Karzai na Bw.Panetta
Rais Karzai na Bw.Panetta

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amelitaka Shirika la kujihami la NATO lirejeshe vikosi vyote vya Kimataifa vilivyo nchini mwake ndani ya vituo vyao.
Ombi hilo alilolitoa wakati wa mazungumzo na Waziri wa Marekani wa Ulinzi, Leon Panetta mjini Kabul linatokea siku tano baada ya askari wa vikosi vya Marekani kuwaua raia 16 wa Afghanistan wakiwa nyumbani kwao. Kutoka Kabul, Hii hapa taarifa ya Quentin Somerville:)
Rais Karzai amemuomba Wazir wa Ulinzi wa Marekani arejeshe vikosi vya Kimataifa katika kambi zao zilizoko nchini Afghanistan, na kukomesha ulinzi wa doria katika vijiji na miji. Amesema kua vikosi vya Afghanistan vina uwezo wa kutekeleza majukumu hayo.
Bado hatua ya kusimamisha shughuli za vikosi hivyo vya Kimataifa ambavyo vilitazamiwa kurejea ndani ya kambi zao ifikapo mwisho wa mwaka 2013.
Katika tukio la kipekee kundi la Taliban limetangaza kua linasitisha mazungumzo na Marekani yaliyopangwa kwa nia ya kuunda afisi ya kisiasa katika Taifa la Ghuba la Qatar pamoja na mpango wa kubadilishana wafungwa.
Taliban wamelaumu matukio haya kwa masharti ya Marekani yasiyokubalika. Ilidhaniwa kua mpango wa kubadilishana wafungwa watano wa Taliban walioko katika gereza la Guantanamo na askari wa Marekani aliyetekwa nyara utafanyika matika majuma machache yajayo.
Tamko hili ni pigo kwa juhudi za kuanzisha mazungumzo ya amani na wakereketwa hao.
Duru za wanabalozi wa Marekani zinasema kua Taliban waliambiwa kua serikali ya Afghanistan sharti iwe sehemu ya majadiliano. Hilo ndio lililozua ubishi wa Taliban ambao hawamtambui Rais Karzai.

No comments:

Post a Comment