TANGAZO


Sunday, March 11, 2012

Profesa Lipumba wa CUF, awasili nchini akitokea Marekani

 Wananchi, mashabiki na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa wamekaa chini, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo, Machi 11, 2012,  wakimsubiri Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, awasili kutoka nchini Marekani, alikokwenda kwa shughuli za kuandaa mipango ya Uimarishaji Uchumi na Demokrasia Duniani. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Baadhi ya umati wa mashabiki na wafuasi wa Chama hicho, ukimsubiri kumuona Profesa Lipumba kwa hamu kubwa, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo, akiwasili nchini akitokea Marekani.


 Baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Chama hicho, wakiwa  wamenyanyua juu picha za Mwenyekiti huyo, Uwanjani hapo.


 Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliokuwepo Uwanjani hapo, wakiangaza huku na kule, kuangalia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka uwanjani hapo.


 Baadhi ya wananchi, mashabiki na wanachama wa chama hicho, wakiwa wamesimama bila kuchoka kwa muda mrefu wakimsubiri Profesa Lipumba awasili uwanjani hapo.


 Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Bara, Julius Mtatiro, akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi hayo.


 Pilika pilika za misafara ya magari, zikipita katikati ya umati wa wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, uwanjani hapo.


 Baadhi ya Wabunge wa Majimbo ya Kisiwa cha Pemba, Rukia Kassim (Viti maalum Chake), Maalim Rashid Ali Omari (Kojani) na Haroub Shamis (Chonga), wakibadilishana mawazo, wakati wakimsubiri Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Lipumba, awasili uwanjani hapo.


Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali, wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kushikana mkono na Mwenyekiti huyo, mara anapowasili uwanjani hapo.


 Baadhi ya Wabunge na viongozi wa juu wa Chama hicho, wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kupeana mkono na Mwenyekiti Profesa Lipumba.


 Wafuasi wa Chama hicho wakiwa wamejazana kwenye maeneo ya Uwanja huo, wakisubiri kwa hamu kumuona Mwenyekiti wao, Profesa Lipumba.


 Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Mustafa Wandwi, akizungumza na waandishi wa habari, uwanjani hapo.


 Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Juma Duni Haji, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mapokezi hayo, uwanjani hapo.


 Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Tabora, Magdalena Sakaya, akizungumza na waandishi wa habari, uwanjani hapo.


 Wafuasi wa Chama hicho, wakiwa wamejipanga kando kando ya barabara inayotoka Uwanja wa ndege kwa ajili ya kumlaki Mwenyekiti huyo.


 Magari yaliyokuwa yamebeba wanachama na wafusi wa Chama hicho, yakiwasili Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi ya Mwenyekiti huyo.


 Msanii Suleiman Msindi 'Afande Sele', kutoka Morogoro, akitumbuiza katika mapokezi hayo kwa wimbo wake wa Karata Dume kabla ya kuwasili kwa Mwenyekiti huyo.


 Profesa Lipumba, akiwapungia wanachama, wapenzi na wananchi waliofika kwa ajili ya kumpokea, akitoka kwenye jengo la VIP, uwanjani hapo.


 Profesa Lipumba, akivishwa koja la maua na binti mdogo, aliyeandaliwa kwa kazi hiyo.


Profesa Lipumba, akijitayarisha kwa ajili ya kumbeba binti huyo, mara baada ya kumvisha koja hilo.

 Profesa Lipumba, akiwa amembeba binti huyo, mara baada ya kumvisha koja hilo, uwanjani hapo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na Makamu wa Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali.



 Profesa Lipumba akipokea tena zawadi ya shada la maua kutoka kwa binti huyo mdogo.


 Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (katikati), akiwa ameshikana mikono kuonesha mshikamano na Makamu wake, Machano Khamis Ali (kushoto) na Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad, mbele ya lango la VIP, uwanjani hapo.


Profesa Lipumba (katikati), akisalimiana na wafuasi, wageni waalikwa pamoja na wananchi waliofika kumpokea uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment