Putin mgombea Urais wa Urusi
OSCE imesema uchaguzi huo ulighubikwa na visa vingi vya udnganyifu na hauwezi kutajwa kuwa huru. Vyama vya upinzani vimeomba kuwepo na maandamano dhidi ya ushindi wa Putin.Taarifa ya shirika hilo imesema japo wagombea waliweza kufanya kampeini zao, masharti na utaratibu wote uliwekwa kuhakikisha Waziri Mkuu Vladimir Putin anatwaa ushindi.
Msemaji wa shirika hilo Tonino Picula ameongeza hakukuwa na ushindani na kampeini za upande wa serikali ziliendeshwa kwa kutumia ralimali za umma. Awali kundi nyingine la waangilizi kutoka Urusi Golos lilisema serikali iliingilia utaratibu wa uchaguzi huku kukiwa na visa vya wapiga kura kulazimishwa kumchagua kiongozi fulani.
Golos imempa Bw. Putin kura chache juu ya asili mia 50 kinyume na matokeo ya tume ya uchaguzi.Hata hivyo katika mkutano wa hadhara, mjini Moscow Bw.Putin alisema alishinda wazi bila udanganyifu.
Vladimir Putin, alirejea wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008 baada ya katiba kumzuia kuwania awamu ya tatu mtawalia kama rais. Ushindi wa sasa utamfanya kusalia madarakani hadi 2018 na anachukua nafasi ya Dmitry Medvedev.
Uchaguzi wa urais nchini Urusi umefanyika huku kukiwa na malalamishi ya udanganyifu katika uchaguzi wa ubunge hapo mwezi Decemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment