TANGAZO


Saturday, March 17, 2012

Mshauri wa Gaddafi akamatwa Mauritania

Wakuu wa Mauritania wanasema kuwa Abdullah al-Sanussi, mkuu wa usalama wa zamani wa Kanali Gaddafi, amekamatwa katika mji mkuu, Nouakchott.

Sanussi

Sanussi - ambaye akionekana ndio msaidizi mkubwa wa Gaddafi - anasakwa na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, kwa uhalifu aliofanya wakati wa vita vya Libya.
Shirika la habari rasmi la Mauritania, linaarifu kuwa Bwana Sanoussi, alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Nouakchott, baada ya kuwasili kutoka Morocco, akitumia paspoti bandia ya Mali.
Wakuu wa Libya wamethibitisha kuwa Bwana Sanussi amekamatwa.
Anatuhumiwa kuwa aliongoza mashambulio dhidi ya raia katika mji wa Benghazi, shina la upinzani dhidi ya serikali, ili kuzima upinzani dhidi ya shemeji yake, Kanali Muammar Gaddafi.
Wananchi wa Libya mjini Tripoli, wamefurahi na habari hizo:
"Hii ni furaha kubwa kwa Walibya.
Natamani tungemkamata sisi wenyewe.
Lolote atalofanyiwa, halitoshi kulipiza yale aliyotenda Sanussi"
Na mwengine alisema:
"Mie nakwambia Sanussi alikuwa ndio sanduku la siri za Gaddafi.
Sanussi ndiye aliyeuwa wafungwa 1200.
Mikono yake ina damu.
Anafaa kuletwa Libya afikishwe mahakamani"

No comments:

Post a Comment