Jeshi la Israil limekuwa likiendelea na mashambulio ya ndege dhidi ya Wapalestina katika Kanda ya Gaza, kwa siku ya tatu mfululizo.
Walioshuhudia matukio hayo wanasema mtoto wa kiume wa miaka 12 aliuwawa karibu na kambi ya wakimbizi ya Jabaliya, na kwamba watu wengine walijeruhiwa katika shambulio la pili dhidi ya mji wa Gaza.
Idadi ya Wapalestina waliokufa sasa inakaribia 20; katika mashambulio makubwa kabisa kutokea Gaza kwa muda wa mwaka.
Wapiganaji wa Kipalestina nao wamerusha makombora dhidi ya Israil.
Mawaziri wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu wanaokutana mjini Cairo, wameishutumu Israil kuwa inazidisha utumiaji nguvu.
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimeeleza wasiwasi na zimesihi utulivu.
No comments:
Post a Comment