Majeshi ya serikali yamefika eneo hilo kutuliza hali. Utawa wa mpito wa Libya unakumbwa na wakati mgumu kudhibiti nchi hiyo baada ya kumuondoa Kanali Muammar Gaddafi mwaka jana.
Ahmed al Hamrouni ambaye zamani alikuwa kamanda wa waasi amesema milio ya roketi imesikika katika barabara kuu huku moshi ukionekana kupaa juu ya uwanja wa ndege wa Sabha.
Serikali ya mpito imewashawishi wapiganaji waliosaidia kumng'oa madarakani kanali Gaddafi kusalimisha silaha na kujiunga na jeshi la taifa.
Mwakilishi wa utawala wa mpito amesema makabiliano yalianza pale wapiganaji wa kabila la Toubou walipojaribu kuiba gari la mpiganaji wa kundi la Sabha.
Msemaji huyo amesema kamati ya maridhiano imeundwa ili kumaliza mapigano.
No comments:
Post a Comment