TANGAZO


Thursday, March 8, 2012

Kampeini ya kukamatwa kwa Kony yaanza

                 
Joseph Kony

Kampeini moja inayoongozwa na kundi la wanaharakati wa Marekani kushinikiza kukamatwa kwa mhalifu wa kivita Joseph Kony imeanza.
Kampeini hiyo inayofanywa kwa njia ya video, imekuwa ikisambazwa kwa kanda ya Video. Kanda hiyo kwa jina 'Invisible Children' inaangazia jinsi waasi wa Lord's resistance Army wamekua wakiwatumia watoto kama wapiganaji wao.
Karibu watu milioni 10 wametazama kanda hiyo ambapo kundi lililoitayarisha limesema inanuia kusaidia kukamatwa kwa Joseph Kony na kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Wakosoaji wa kanda hiyo wamehoji agenda ya kundi hilo ambapo baadhi ya wasanii mashuhuri akiwemo mwanamziki Rihanna na P Diddy wametoa hisia zao.
Kony na wapiganaji wake wamelaumiwa kutekeleza dhuluma za kibinadamu katika nchi nne ikiwemo Uganda, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan Kusini na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Mnamo Oktoba mwaka jana Rais Barack Obama alitangaza kutuma kikosi maalum cha jeshi la Marekani nchini Uganda ili kusaidia kumnasa Josph Kony.
Kiongozi huyo pamoja na washirika wake wa karibu waliwekewa vibali vya kukamatwa na mahakama ya ICC hapo mwaka 2005.
Vita vya LRA kaskazini mwa Uganda vimeendelea kwa zaidi ya miongo miwili ambapo kundi hilo linatetea haki za jamii ya Acholi.LRA imelaumiwa kwa kuwateka nyara watoto wavulana na kuwafanya wapiganaji na wasichana hufanywa watumwa wa ngono.

No comments:

Post a Comment