TANGAZO


Monday, March 19, 2012

Mkurugenzi JB Belmont, aukwaa Uenyekiti wa Jumuiya ya Waganda nchini

Justus Baguma, akizungumza. akwa na Balozi Ibrahim Mukiibi
Na Eben-Ezery Mende
MFANYABIASHARA mashuhuri nchini, Justus Baguma (JB) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Watu wa Uganda Wanaoishi nchini Tanzania (AUCT) nafasi ambayo awali ilikuwa ikiongozwa na George Kanuma.
Uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita uliwafanya viongozi wawili waliokuwa kwenye uongozi wa awali kurudi huku wengine watatu wakianguka.
Awali Buguma alikuwa mweka hazina wa chama hicho nafasi ambayo sasa imechukuliwa na Alex Mwijuka, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikaenda kwa Hellen Tusiime nafasi ambayo awali ilikuwa inashikiliwa na Jimmy Sekiito.
Nafasi ya Katibu Mkuu imeendelea kushikiliwa na Dorothy kalema, na nafasi ya katibu mratibu wa matukio ya chama ikatwaliwa na Tony Kiyita nafasi iliyokuwa ikiongozwa na Dennis Busulwa.
Nafasi nyingine za uongozi ziliongezwa baada ya kuonekana kuwepo uhitaji huo ambazo ni mratibu wa walimu iliyochukuliwa na Muwonge Ismail, uratibu wa masuala ya kibiashara, Lubega Thomas, uratibu wa masuala ya wanafunzi, Akol Adrian na mratibu wa masuala ya uhamiaji, Mushagara Aggrey.
Viongozi wengine ni msimamizi wa sekta ya michezo, Ivan Kakooza, sekta ya afya, Dk. Richard, uhusiano, Patrick Kigongo, sekta ya vijana, Norah katumba, mratibu wa masuala ya wanawake, Josephn kato na mratibu wa umoja wa chama hicho, Josheph Nuwamanya.
Chama hicho kilianzishwa mwaka 2010 na uchaguzi uliofanyika ni wa pili tangu kuanzishwa kwa chama hicho kutokana na mwongozo wa katiba ambao unabainisha kuwa uchaguzi unatakiwa kufanyika kila baada ya miaka miwili.

No comments:

Post a Comment