Mahakama ya Kimataifa kuhusu haki [International Court for Justice] inasikiliza ombi la kumtaka rais wa zamani wa Chad Hissene Habre afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za uhalifu wa kivita zinazomkabili.
Bw Habre, 69, anatuhumiwa kwa mauaji ya mateso kwa makumi ya maelfu ya wapinzani wake kati ya mwaka 1982 na 1990 – tuhuma ambazo anazikanusha.Amekuwa akiishi uhamishoni nchini Senegal tangu apinduliwe madarakani mwaka 1990 na alikamatwa mwaka 2005 lakini hajawahi kushtakiwa.
Senegal awali ilikataa maombi manne ya kusafirisha mpaka Belgium akashtakiwe.
Belgiuji iliomba mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa kuiamuruSenegalkutimiza wajibu wake chini ya sheria ya kimataifa ama imhukumu au asafirishwe kwendaBrusselskujibu mashtaka yanayomkabili.
Kesi hiyo inahusu ‘kuchukua msimamo dhidi ya makosa makubwa katika uhalifu mkubwa kwenye sheria za kimataifa’, mwakilishi wa Ubelgiji Paul Rietjens alisema wakati wa ufunguzi, shirika la habari la AP linaripoti.
Kesi itaanza kusikilizwa tarehe 21 Machi mjini The Hague, makao makuu ya Mahakama hiyo.
Mwakilishi waSenegalanatarajiwa kufungua kesi yake siku ya Alhamisi.
Akijulikana kama ‘Pinochet Afrika’, Bw Habre alishtakiwa mwaka 2005 na Belgiumkwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mateso.
Hissene Habre ni nani?
- Alizaliwa 1942 kutoka kabila la wafugaji wa Toubou kaskazini mwaChad
- Alipewa ufadhili masomo ya sayansi ya siasa nchini Ufaransa
- Alikuja kujulikana duniani kwa mara ya kwanza mwaka 1974 wakati waasi wake wa FAN walipowakamata mateka wazungu watatu kwa kutaka kikombozi cha fedha na silaha.
- Alichukua madaraka mwaka 1982 ikituhumiwa kusaidiwa na shirika la ujasusi la Marekani-CIA na kupinduliwa na Rais wa sasa Idriss Deby mwaka 1990.
- Anatuhumiwa kuyatesa mfululizo makundi ya watu ambao hakuyaamini
- Bwawa la kuogelea la zamani lilitumiwa kama gereza la kificho ambako waathirika waliteswa kwa kushtuliwa na nyaya wa umeme na mateso mengine na makubwa.
Mwezi Januari mahakama ya Senegal ilikataa ombi la Ubelgiji ya kumsafirisha Bw Habre Ubelgiji.
Wakati huo Rais wa Senegal Abdoulaye Wade alisema alitarajia kusafirishwa huko kungefanyika mara moja.
Katika mashtaka ya Mahakama ya Haki ya Kimataifa,Senegal bado ina nia ya kumshtaki Bw Habre, kwa mujibu wa kampeni za shirika la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch.
No comments:
Post a Comment