TANGAZO


Wednesday, March 28, 2012

Chelsea yanusa nusu fainali

Salomon Kalou aifungia Chelsea bao

Bao la Salomon Kalou iliisaidia timu ya Chelsea kuingiza mguu mmoja katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mabinwa bara ulaya baada ya kuwachapa wenyeji wao Benfica ya Ureno.
Mwamba huyo wa Ivory Coast alifunga bao hilo la pekee katika daikia ya 75 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Fernando Torres ambaye nae katika mechi hii alikuwa katika hali nzuri.
Hapo awali Kalou alipoteza nafasi kadhaa za kufungo mabao.
Kauli ya Drogba iliyodaiwa awali na kocha wa Benfica kuwa ilikuwa ya kejeli kwa timu yake na kutaka kauli hiyo ijibiwe kwa kipigo kwa Chelsea, goli la Kalou lilionekana kuipa nguvu zaidi kauli hiyo na huenda hata kocha mwenyewe Jorge Jesus ameumia zaidi kwani dhamirra yake ya kuwaadhibu Chelsea haikutokea.
Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo katika kuhakikisha anapata ushindi, aliwatumia wachezaji wake wenye uzoefu mkubwa na uchezaji wa timu za Ureno.
Wachezaji wa zamani wa Benfica kama vile kina David Luiz, Ramires, Raul Meireles na Paulo Ferreira ndio waliopewa kibarua cha kuihangaisha timu yao ya zamani.

Apoel Nicosia 0-3 Real Madrid

Nao vijana wa Morinho, Real Madrid wameifanyia mauaji Apoel ya Nicosia kwa kuishushia kipigo cha magoli matatu kwa bila nyumbani kwao.
Alikuwa Kaka kiungo mshambuliaji akitokea benchi, ndiye aliyechochea ushindi huo dhidi ya Apoel ambao waliikatalia Real Madrid kufunga bao hadi kipindi cha pili.
Ilikuwa ni krosi ya Kaka kwa Karim Benzema iliyozaa goli la kwanza na Kaka naye akipokea krosi ya Marcelo kufunga goli la pili na Benzema akikamilisha karamu ya magoli kwa Real Madrid kwa kufunga goli la tatu akipokea pasi maridadi ya Mezut Ozil.

No comments:

Post a Comment