TANGAZO


Monday, February 6, 2012

Yaliyojiri Bungeni leo

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo, mjini Dodoma.  (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)


 Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akijibu maswali ya wabunge kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini  na uondoaji wa tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea kwenye baadhi ya maeneo nchini pia kufafanua kuwa Serikali inaendelea na mikakati ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma ya umeme katika maeneo yasiyo na huduma hiyo pamoja na kuimarisha uzalishaji wa umeme wa uhakika katika Gridi ya Taifa kupitia vyanzo mbalimbali.


 Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR –Mageuzi), David Kafulila akichangia bungeni, kuhusu namna bora ya  ukusanyaji wa mapato kupitia kodi zinazotozwa kwenye makampuni ya simu nchini, ili kuongeza mapato ya Serikali leo, mjini Dodoma.


 Waziri na Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hadji Mponda (kushoto), akimweleza jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bunge jana mjini Dodoma. Nyuma yao ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia. (Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)


 Naibu Waziri wa Fedha  Gregory Theu (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher  Chiza, nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodom.


Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wabunge mara baada ya kumalizika kwa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Davidi Kafulila (wa pili kutoka kushoto) kutoka Kigoma kusini na Mbunge Said Arfi wa Mpanda Mjini.

No comments:

Post a Comment