Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Kata za Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, alipowasili eneo hilo, kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la jengo la ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati akiwa katika ziara yake wilayani humo leo, Januari 27, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunua pazi ili kuzinduz jiwe la msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, katika ziara yake hiyo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na viongozi wa Wilaya ya Korogwe, wakikagua ukumbi na Ofisi za jengo la Halmashauri ya Korogwe, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo hilo leo wilayani humo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa mpunga, kuhusu kilimo hicho cha umwagiliaji, wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya Skim Mamlaka ya Mji wa Mombo, jana Januari 26, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikagua mitaro ya maji yanayotumika kumwagilia mashamba ya mpunga ya mpango huo, mjini Mombo, jana.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma ujumbe ulioandikwa na vijana wa Harakati za Mazingira, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mamlaka ya Mji wa Mombo, kwa ajili ya kuwahutubia wananchi, akiwa katika ziara yake hiyo. Kulia kwake ni mkewe, Mama Zakhia Bilal na (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa. (Picha na Muhidi Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kombe, kiongozi wa timu ya Mombo Shooting, Mohamed Dassa, kwa ajili ya timu hiyo, iliyopanda daraja kutoka Ligi ya Ngazi ya Wilaya na kuingia Ligi Ngazi ya Mkoa. Kombe hilo pamoja na vifaa vya michezo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
No comments:
Post a Comment