TANGAZO


Thursday, January 26, 2012

Liverpool yatinga fainali ya Carling

 
Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish alisema ushindi wa klabu yake dhidi ya Man.City ni kwa ajili ya mashabiki. Liverpool iliishinda Man.City katika nusu fainali ya Kombe la Carling jumla ya mabao 3-2.

Kenny Dalglish
Dalglish awazawadia ushindi mashabiki
Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 16 kwa Liverpool kutinga fainali kwenye uwanja wa Wembley baada ya kutoka 2-2 kwenye uwanja wa Anfield. Ikumbukwe kua Liverpool ilishinda 1-0 katika mchuano wa kwanza wiki mbili zilizopita kwenye uwanja wa Ettihad mjini Manchester.
Ushindi huo unatokea wakati ambapo wamiliki wa klabu hio kutoka Marekani ndio kwanza wameanza kuelewa mfumo wa soka ya England pamoja na sakata la ubaguzi wa rangi lililosababisha mshambuliaji wa klabu hio Luis Suarez kubanwa na sheria ya chama cha mpira England.
Licha ya usajili ulioonekana kua mzuri pamoja na kumleta kocha wao wa zamani Dalglish, Liverpool bado haijafikia viwango vilivyotarajiwa na mashabiki wake.
Klabu hio haijashinda kombe lolote tangu lile la FA la mwaka 2006 ilipoinyuka West Ham United mjini Cardiff na haijafuzu kushiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa misimu miwili iliyopita.
Wakati huu klabu hii imo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ikidorora kwa pointi sita nyuma ya nne bora, baada ya kufungwa 3-1 na Bolton jumamosi iliyopita.
Kufuatia ushindi wa 1-0 katika duru ya kwanza kwenye uwanja wa Etihad, City ndiyo iliyoliona lango kwanza kupitia shuti ya Nigel de Jong kutoka umbali wa yadi 25.
Lakini waliweza kurudisha bao hilo kupitia mkwaju wa peneti ya kutatanisha kufuatia beki Micah Richards kuonekana kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari. Nahodha Steven Gerard alifyatua kombora lililompita golikipa wa City kama upepo.
Lakini City wakarudi kufunga tena kupitia Edin Dzeko ingawa Craig Bellamy aliyehangaika sana kipindi cha mechi nzima akitafuta ushindi, akaipatia Liverpool bao la pili na la ushindi dakika 16 kabla ya kipenga cha kumaliza mechi.

No comments:

Post a Comment