TANGAZO


Thursday, January 26, 2012

JICA yasaidi vIfaa vya kupunguza maambukizi ya VVU nchini

 Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wawakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa hafla ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini  uliofadhiliwa na Serikali ya Japan jijini Dar es salaam jana. (Picha na Aron Msigwa - Maelezo)


 Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wawakili kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika hafla.


 Mwakilishi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kimaendeleo la Japan (JICA), Yukihinde Katsuta, akitoa maelezo juu ya ukamilishwaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini, Tanzania uliofadhiliwa na Serikali ya nchi hiyo kwa lengo la kupunguza maambukizi ya VVU, sanjari na  usambazaji wa vifaa vya kupimia maambukizi hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika utoaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni akimkabidhi Zawadi iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi  wa Jamii, mwakilishi mkuu wa JICA wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini  uliofadhiliwa na Serikali ya Japan jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).

No comments:

Post a Comment