Pages

Saturday, March 12, 2016

MOJA KWA MOJA:Norwich dhidi ya Manchester City

Na Ligi kuu ya England inaendelea tena jumamosi hii kwa michezo mitatu,Norwich City wanawakaribisha Manchester city,Bournemouth dhidi ya Swansea city na Stoke ni wenyeji wa Southampton
17.31pm:Aguero achenga moja mbili lakini apiga mnazi pale na mpira unatoka nje
17.30Pm:Dakika ya lala salama Manchester City inajaribu kutafuta bao.
17.28pm:Norwich wanafanya shambulio hapa lakini linatoka nje .lilikuwa bao la wazi
17.24pm:Norwich wamelemewa hapa inaonekana City wanatafuta bao kwa udi na uvumba
17.23pm:Dakika za lala salama Norwich 0-0 Manchester City
Michael Olunga
17.01pm:Kocha wa timu ya IF Djurgarden Per Pelle Olsson amemsifu aliyekuwa mshambuliaji wa kilabu ya Gor Mahia Michael Olunga baada ya kufunga bao jingine katika mechi ya kirafiki iliochezwa siku ya ijumaa.Olunga alifunga bao katika kipindi cha kwanza cha mchezo lakini bao hilo halikutosha kwani Djurgaden walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Elfsborg.
Akizungumza baada kipenga cha mwisho, mkufunzi wa klabu hiyo Olsson alimsifu mchezaji huyo wa zamani wa K'Ogalo akimtaja kuwa mshambuliaji kamili.
''Olunga ni mchezaji mzuri sana.Pia anaonyesha kwamba ana uwezo wa kusoma mechi.Ni mchezaji mwenye kasi licha ya ukubwa wake,kwa hivyo kwa jumla atatusaidia sana kwa upande wetu''.
16.58pm:Raheem Starling ajitayarisha kuingia kwa upande wa Manchester City huku Wlfiried Bony akitoka
16.52pm:Aguero avamia lango la Norwich anakwenda lakini anaangushwa nje ya eneo hatari
Aguero
16.45pm:Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi huku Norwich wakishambulia lango la City
16.32pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kinakamilika hapa huku Norwich wakionekana kutawala dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.Norwich 0-0 Manchester City
16.25pm:lalalala shambulizi linapiga chuma cha goli la Manchester City do.Karibia Norwich wajiweke kifua mbele
Wachezaji wa Norwich
16.23pm:Norwich sasa inatawala mpira huku Manchester City wakifukuza kivuli
16.22pm:Hatari katika lango la Manchester City.kona
16.21pm:Wachezaji wa Norwich wajaribu kulivamia lengo la City lakini wapi bahati haijasimama
16.14pm:Aguero lalala anaukoamchezaji wa Norwich .Aguero akosa bao la wazi hapa.
16.13pm:Norwich sasa imeanza kufungia kucha na sasa inashambulia lango la City.
Makabiliano
16.11pm:Mkwaju wa adhabu kuelekea City.lakini mchezaji wa Norwich amchezea visivyo kipa na mpira unapigwa kuelekea Norwich.
16.10pm: Dakika ya 25, Norwich 0-0 Manchester City
16.06pm:Manchester City yavamia lango la Norwich kama nyuki,hapa na pengine huenda haitachukua mda .Kumbuka iwapo City watashinda basi wataingia katika nafasi ya tatu juu ya Arsenal ambao wana kibarua na Watford siku ya jumapili
15.55pm:Mancity wanaanza mechi kwa kasi huku Sergio Aguero na Fernandinho wakishirikiana hapa
Mancity
Kikosi cha Mancity
Norwich City
Kikosi cha Norwich
15.45pm:Norwich vs Man City
Mechi inaanza.

No comments:

Post a Comment