Korea Kusini inasema kuwa kuna dalili kuwa Korea Kaskazini inapanga majaribio zaidi ya makombora hususan makombora ya masafa marefu.
Maafisa wa ulinzi wamekuwa wakilishauri bunge mjini Seoul baada ya Korea kulifanyia jaribio bomu la nyuklia mwishoni mwa wiki.
Korea Kusini imejibu kwa kufanya majaribio kwa kurusha makombora kwa kutumia ndege na kutoka ardhini.
Marekani imeonya kuwa tisho lolote kwake na kwa washirika wake litajibiwa vikali kijeshi.
Korea Kusini inasema kuwa ililifanyia majaribio bomu la haidrojeni ambalo linaweza kuwekwa kwa kombora la masafa marefu.

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura baadaye leo kujadili hatua za kuchukua.
Chang Kyung-soo, ambaye ni afisi kutoka wizara ya ulinzia aliliambia bunge, "tunaendelea kuona dalili za uwezekano wa makombora zaidi ya masafa marefu. Pia tunaweza kutabiri kuwa Korea Kaskazini huenda ikarusha kombora la masafa marefu.
- Korea Kusini yafanya majaribio ya makombora kujibu majaribio ya Korea Kaskazini
- Bomu kubwa la vita vya pili vya dunia kuharibiwa Ujerumani
Wizara hiyo pia ililiambia bunge kuwa huenda Marekani ikapeleka manowari ya nyuklia ya kubeba ndege katika rasi ya Korea.

No comments:
Post a Comment