TANGAZO


Monday, December 7, 2015

Newcastle yainyuka Liverpool ligi kuu England

Georginio Wijnaldum


Image copyrightReuters
Image captionGeorginio Wijnaldum alisaidia katika kupatikana kwa bao la kwanza

Ligi kuu ya soka ya England iliendelea tena jana kwa mchezo mmoja pekee uliopigwa katika dimba la St James Park wenyeji Newcastle wakiwakaribisha majogoo wa London Liverpool, ambapo Newcastle walifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa bao 2-0.
Dakika ya 69 ya mchezo katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Georgino Winaldum, Martin Skrtel wa Liverpool alijikuta akijifunga katika harakati za kuokoa mpira huo.
Na dakika ya 93 ndani ya muda wa nyongeza Wina-Naldum aliamsha shangwe St James Park kwa kuandika bao la pili.
Kwa Ushindi huo sasa Newcastle wamekwea hadi nafasi ya 18 wakiwa na pointi 13 juu ya Sunderland na Aston Villa ambao wanaburuta mkia katika msimamo wa ligi.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo Jumatatu kwa mchezo mmoja tu ambapo Everton watawaalika Crystal Palace.

No comments:

Post a Comment