TANGAZO


Tuesday, January 13, 2015

Ulinzi wa Albino Tanzania, Waziri Chikawe azungumza na waandishi wa habari

*Apiga marufuku waganga wapiga ramli
*Jeshi la Polisi launda kikosi kazi na Tas kuwalinda albino
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipozungumza nao, kuhusu kuundwa kamati ya pamoja na Chama cha watu wenye ulemevu wa ngozi (albino) Tanzania (Tas) kwa ajili ya kuilinda jamii hiyo nchini dhidi ya vitendo vya ukatili. Katikati ni Mwenyekiti wa chama hicho, Ernest Kimaya na kushoto ni Ofisa Habari wa chama, Josephat Torner. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wapigapicha na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo, Dar es Salaam leo.
Wapigapicha na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, akizungumza na wa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuwalinda albino dhidi ya uhalifu. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP, Ernest Mangu.
Mwenyekiti wa chama hicho, Ernest Kimaya, akizungumza katika mkutano huo leo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ILI kukomesha tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) Jeshi la polisi nchini kwa kushirikiana na chama cha chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) limeandaa operesheni kali ya kuwakamata  waganga wa jadi wanaojihusisha  kwa namna moja au nyingine kwa kuwaagiza wateja viungo vya watu hao.
Aidha, Jeshi hilo limetangaza kuwa litapita mtaa hadi mtaa ili kubaini watu wanaohusika na suala hilo ambapo litawakamata kutokana na ushirikiano watakaooneshwa toka kwa wananchi.

Pia jeshi hilo limesema litaunda timu ya watu 6 ambapo jeshi la polisi 4 na Tas 2 kwa ajili ya kuhakikisha wanakomesha tatizo hilo linakomeshwa uonevu huo na madahara wanayopata watu wenye ulemavu wa ngozi.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe alisema watashirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kupitia kata, tarafa na mikoa ili kupata taarifa.
Alisema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha wahusika wanakamatwa kutokana na kufikishwa kwenye vituo vya sheria husika ili kuchukulia hatua.
"Tatizo kubwa linalosababisha mauaji haya ni kutokana na watu kutokua na elimu sahihi na elimu ya dini hivyo mashirika ya dini yatoe elimu kwa jamii kuhusiana na masuala kama hayo,"alisema.

Chikawe alisemawamemua kupiga marufuku wapiga ramli kutokana na kwamba ndio chanzo kikubwa kinachopelekea watu kuua albino na kuwapelekea viungo hivyo kwa nia ya kutaka utajiri na mambo mengine.

Akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na wandishi wa habari Chikawe alisema watashirikiana na Tamisemi kutokana na kuwa wao ndio wahisika wakuu katika utendaji hivyo wanajua watu wanaoishi katika maeneo mbalimbali.

Alisema kutokana na onyo hilo kama watu hao wataendelea watafikishwa mahakamani hataka iwezekanavyo pia watafanya kampeni kubwa ya kutoa elimu kwa wabnanachi ili tatizo liweze kuisha.

"Tunataka tatizo liishe, kwa sasa hali ni nzuri tofauti na mwanzoni ambapo tumekamata watu 15 waliohisika kwenye utekaji wa mtoto Mkoani Mwanza tunawafanyia mahojiano ili nao waweze kutaja wengine waliohusika,"alisema.
Akizungumzia operesheni hiyo alisema itaanza baada ya wiki mbili katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Tabora, Shinyanga na kufuatiwa na Kagera, Sumbawanga, Mara na Mbeya ambapo matukio hayo yamekua yakitokea mara kwa mara.

Aidha alisema kikosi watakachounda kitakuwa ni kwa ajili ya kusikiliza kesi zote za nyuma ili kupata ushahidi kutokana wa kesi nyingine za nyuma zilizofutwa kutokana na kukosa ushahidi.


Kwa upande wake Rais wa (Tas), Joseph Tona alisema kuwa timu hiyo itawasaidia kupata taarifa mbalimbali toka kwa wananchi hivyo aliwataka wananchi kutoa ushirikano ili kudhibiti tatizo hilo.


Hata hivyo aliwataka wananchi kutoa taarifa na kwamba hakuna atakayetajwa jina ambapoi watafikishwa katika vituo vya polisi ka uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment