TANGAZO


Tuesday, January 13, 2015

TBL yakagua miradi ya visima inavyofadhili Bagamoyo mkoani Pwani

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) akielekeza jambo kwa fundi alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi wa uchimbaj wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki.Miradi hiyo itagharimu sh. mil. 51.7.
Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima vya maji unaofafadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia), akitoa maelekezo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo, Pwani. TBL inafadhili miradi hiyo kwa gharama ya sh. mil. 51.7. 
Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akimuonesha Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto) moja ya mabomba yatakayotumika kwa ajili ya kuvutia maji kutoka katika visima vilivyochimbwa katika mradi wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Manzini B, wilayni Bagamoyo Pwani mwishoni mwa wiki. TBL inafadhili miradi hiyo kwa gharama ya sh. mil. 51.7. (Picha zote na Mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment