Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala Ndugu Theresia Mbando (wa
tatu kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (wa nne)
nje ya jengo la Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kupokea maandamano ya
wanafunzi wa shule za msingi za Dar es Salaam wakati wa sherehe ya
uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa huo tarehe
12.6.2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam wakiwa
wamebeba mabango yenye picha na ujumbe mbalimbali wakati wa sherehe za
uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar zilizofanyika kwenye
ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mchezo wa sarakasi iliyokuwa
ikichezwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar wakati wa sherehe
ya uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Ndugu Raymond Mushi (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya E &
D, Ndugu Demere Kitunga (kushoto) wakati wakielekea kwenye ukumbi kwa
ajili ya sherehe za uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar
tarehe 12.6.2014.
Baadhi
ya watoto walioshiriki uzinduzi wa tamasha la vitabu mkoani Dar es
Salaam wakiwa wanasoma baadhi ya vitabu na majarida ya watoto wakati wa
sherehe hizo kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha moja ya kijarida cha hadithi
kwa ajili ya watoto alichokichagua kwa ajili ya kuwasomea hadithi watoto
wakati akizindua rasmi Tamasha la vitabu vya watoto kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa hapa Dar Es Salaam.
Mgeni
Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu kwa wanafunzi wa
Shule za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mama Salma Kikwete
akiongea na wanafunzi wakati wa uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Makumbusho
terehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mtoto Edda Kasika kutoka
Shule ya Msingi Maktaba tuzo kwa kushika nafasi ya pili katika uandishi
wa insha katika Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa
tamasha la vitabu kwa watoto tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi washindi wa insha na mchapishaji wa vitabu bora vya watoto na
wageni waalikwa mara baada ya kuzindua rasmi tamasha la vitabu vya
watoto wa shule tarehe 12.6.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia maonyesho ya vitabu, vijarida na
kazi mbalimbali zilizokuwa zikionyeshwa na wanafunzi wa shule za msingi
mkoani Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu
vya watoto tarehe 12.7.2014.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu
Theresia Mbando mara baada ya kuzindua rasmi Tamasha la vitabu vya
watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
jana, terehe 12.6.2014. (Picha zote na John Lukuw)
No comments:
Post a Comment