Marekani imeituhumu Sudan kwa kufanya mashambulio dhidi ya raia wake katika majimbo ya Kordofan kusini na Blue Nile .
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ,
Samantha Power amelaani mashambulio hayo ambayo alisema yalilenga shule
na hospitaliBi Power amesema kuwa tangu mwezi April mamia ya makombora yamekuwa yakirushwa kwa ndege za kijeshi za Sudan katika miji na vijiji katika kanda hiyo .
Zaidi ya watu milioni wameripotiwa kuyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi hayo . Balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa hakujibu kauli ya Bi Power.
Mapema juma hili, mashirika ya misaada yaliliandikia baraza la usalama la umoja wa mataifa, umoja wa Afrika pamoja na jumuiya ya nchi za kiarabu yakitaka mashambulizi dhidi ya raiya yasitishwe na serikali ya Sudan.
Bi Power aliilaani kwa matamshi mazito zaidi mashambulizi ya serikali ya Sudan katika eneo hilo.
Waasi kutoka katika kabila lililo na watu wachache katika sehemu hiyo wamekuwa wakipigana na majeshi ya serikali kwa miaka mitatu katika vita ambavyo vimeathiri zaidi ya watu milioni moja kwa mujibu wa umoja wa
Bi Power alilinganisha mbinu za kivita za serikali hiyo na zile zinazotumika katika vita vilivyoharibu sehemu ya Magharibi mwa Darfur, ambapo serikali ililaumiwa kwa kufanya mashambulizi kwa misingi ya kikabila.
“Marekani inatoa wito kwa makundi yote yaliyojihami kusimamisha vita dhidi ya raiya na kutii sharia za kimataifa,” alisema.
No comments:
Post a Comment