TANGAZO


Friday, June 13, 2014

Jamaica kulegeza sheria kuhusu Marijuana


Serikali inataka kuruhusu matumizi ya Bangi kwa misingi ya kidini, kisayansi na kimatibabu

Serikali ya Jamaica imetangaza kuwa inatafakari upya mipango ya kufanyia mageuzi sheria zake za kukabiliana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Waziri wa sheria Mark Golding, amesema kuwa baraza la mawaziri linaunga mkono pendekezo kuwa kiwango kidogo zaidi cha Bangi, kitakachoruhusiwa kwa mtu kumiliki kitakuwa gramu 57.
Bwana Golding amesema kuwa Marijuana itaweza kuhalalishwa kwa kiwango kidogo kwa sababu za kidini , matibabu na utafiti wa kisayansi.
Inatarajiwa kuwa bunge la nchi hjiyo litaweza kupitisha mswada huo ifikapo mwezi Septemba.
"nataka nisisitize kuwa magezi yanayopendekezwa kufanyiwa sheria hayalengi kuhalalisha matumizi ya Bhangi kwa sababu ya kujiburudisha,'' alisema bwana Golding.
Lengo ni kuwezesha muelekeo mzuri wa kukabiliana na visa vya watu wanaopatikana wakiwa na viwango vidogo vya Bangi.
Wandishi wa habari wanasema mipango ya serikali ni kama ushindi kwa watu wa Rastafaria ambao wanaamini kuwa Ganja ni kitu kitakatifu.
Mageuzi ya hivi karibuni katika nchi kama vile Uruguay au majimbo kadhaa nchini Marekani, kama vile Colorado, yameweza kushinikiza zaidi kampeini ya wakulima wa Bangi pamoja na sheria kuhalalisha matumizi ya mmea huo.
"sio jambo zuri kuendelea kudhibiti matumizi ya Bangi au kuendelea kusisitiza sheria inayowazuia watu kumiliki Ganja kwa sababu za kimatibabu,'' asema bwana Golding
Bi Angela Brown Burke, meya wa mji Kingston, alinukuliwa akisema : "muda umewadia kutoa fursa kwa wajamaica kunufaika kutokana na biashara za Marijuana.

No comments:

Post a Comment