TANGAZO


Saturday, August 18, 2012

Rais Kikwete, Joyce Banda wa Malawi, wakutana Msumbiji

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Malawi, Joyce Banda nchini Msumbiji, ambapo wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupitia Kamati Maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo. (Picha na Freddy Maro)
Rais Kikwete, Joyce Banda wakiwa wameshikana mikono

MAPUTO, Msumbiji

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na mwenzake wa Malawi, Joyce Banda, wamekutana nchini Msumbiji na kufanya mazungumzo mafupi yenye nia ya kumaliza mgogoro wa mpaka unaohusisha nchi zao.

Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Joyce Banda walikubaliana kumaliza mgogoro huo Kidiplomasia, kupitia Kamati Maalumu iliyoundwa kushughulikia sakata hilo linalohusu mpaka sehemu ya Ziwa Nyasa.
Kupitia mazungumzo hayo, Rais Kikwete alisema: "Mimi ndiye Amir wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, sijapanga wala kutoa agizo la vita...
"Wanasiasa na waandishi wa habari wa mataifa yote mawili, wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki na chokochoko miongoni mwa raia, hasa wa maeneo ya mpakani.
Rais Kikwete akaenda mbali zaidi kwa kuwataka Watanzania na Wamalawi, wayapuuze maneno hayo, badala yake waache diplomasia ifanye kazi yake.

No comments:

Post a Comment