TANGAZO


Friday, August 10, 2012

Airtel yafuturisha wateja wake, jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi  Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangalloor (wa pili kushoto), akichukua chakula pamoja na baadhi ya wateja wao wa Makampuni katika hafla ya futari waliyowaandalia Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana.

Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki (kulia), akimwekea chakula mmoja wa wa teja wao katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa Makampuni katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wateja wa Airtel, wakipakua mlo wa futari katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Airtel katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana.

Ofisa Mauzo wa Wateja wakubwa wa Airtel Tanzania, Mariam Ikoa (kushoto), akimkabidhi zawadi Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao wa Makampuni katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Matawi na Utawala wa Shirika la Nyumba (NHC), Raymond Mndolwa na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Sam Elangallor.

No comments:

Post a Comment