Mkurugenzi wa Cosmo Entertainment, Benji Cosmo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salam jana, kuhusu Tamasha la Caribbean kwa ajili ya kuadhimisha, Bob Marley Day 2012, litakalofanyika Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam kesho Mei 19. Kushoto ni msanii Jhikoman wa Afrikabisa band na kulia ni msanii Ras Innocent Nganyagwa. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo, Jahson wa kundi la Kandamoja Root, akighani moja ya nyimbo za kundi hilo, wakati Mkurugenzi wa Cosmo Entertainmet, Benji Cosmo (katikati), alipokuwa akizungumza kuhusu tamasha hilo, litakalofanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kesho.
Msanii Ras Magere wa kundi la Warriors from Tunaweza band, akighani moja ya nyimbo zao watakayoitumia kwenye tamasha hilo kesho, Kijitonyama viwanja vya Posta. Kushoto ni muandaaji wa tamasha hilo, Benji Cosmo.
Msanii Ras Innocent Nganyagwa wa kundi la 'The Innocent People Band', akighani wimbo wake unaoitwa, 'Kafara ngapi', wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari. Katikati ni muandaaji wa tamasha hilo, Benji Cosmo na kushoto ni mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo, msanii Jhikoman.
Kundi la 'Warriors From the East', akionesha manjonjo yao kwa kughani moja ya wimbo wao kwenye ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment