TANGAZO


Thursday, May 17, 2012

Serengeti Bia yawaandalia wanablogi semina ya maadili, miiko ya kazi na masharti ya mikataba

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda, akitoa mada kwenye semina ya uendeshaji wa mitandao ya Eletroniki ya upashanaji habari katika kutekeleza maadili, Sheria pamoja na miiko ya utekelezaji wa mikataba ya udhamini kutoka kwa Makapuni watangazaji. Semina hiyo, iliandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya Kampuni hiyo, Masaki, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Blogu ya Mtaa kwa Mtaa, Othman Michuzi. (Picha na Kassim Mbarouk)

Wakurugenzi na waendeshaji wa Blogu mbalimbali nchini, wakimsikiliza Mkurugenzi wa  Mawasiliano wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda wakati alipokuwa akiwasilisha mada mbalimali kwa wanablugu hao jijini leo.
 Wakurugenzi na waendeshaji wa Blogu mbalimbali, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina yao hiyo leo.

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru, akifafanua jambo kwa Wakurugenzi na waendeshaji wa mitandao ya Blogu na Tovuti, wakati wa semina yao ya Maadili, Miiko na Sheria katika kutekeleza mikataba ya udhamini wa Makampuni wa mtandao hiyo ya upashanaji habari. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda.

 Wanablogu mbalimbali wakifuatilia kwa maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa kwenye uwasiliashaji mada katika semina hiyo.

 Mmoja wa Wakurugenzi wa blogu, Joachim Mushi, akiuliza swali kwa muwasilishaji mada, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiana wa SBL, MTeddy Mapunda (hayupo pichani), wakati wa semina hiyo.

 Mkurugenzi Mwendeshaji wa blogu hii, www.bayana.blogspot.com, Kassim Mbarouk, akikabidhiwa cheti na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru,  baada ya kuwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo, iliyotayarishwa na kuendeshwa na Kampuni hiyo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiana wa SBL, MTeddy Mapunda.

  Mwendeshaji wa Blogu ya Mtaa kwa Mtaa Othman Michuzi kushoto akipokea cheti chake.

 Mkurugenzi wa blogu ya Nkoromo blog, Bashir Nkoromo akikabidhiwa cheti chake cha ushiriki na Mkurugenzi wa Masoko Ephraim Mafuru.

 Mroki Mroki wa blogu ya Father Kidevu (kushoto), akipokea cheti chake.

 Josephat Lukaza wa Lukaza blogu, akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru.

 Japhet Olelengine wa Kampuni ya R&R, akipokea cheti chake baada ya kushiriki semina hiyo.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya R&R, Caroline Gul (kushoto), akipokea cheti chake.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru (kulia waliokaa) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa kampuni hiyo,Teddy Mapunda (kushoto waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waeneshaji wa blogu nchini, mara baada ya kumalizika semina yao na kupokea vyeti vyao leo, Mkao Makuu ya Kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment