TANGAZO


Sunday, January 22, 2012

Makamu wa Rais na Shughuli za Maendeleo Kusini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini, Salum Baruani, wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari Mnolela, Lindi kwa ajili ya kuzindua Jengo la Utawala la Shule hiyo, jana Januari 21, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili, wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari ya Mnolela, alipofika kuzindua jengo la Utawala la shule hiyo, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana, Januari 21, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo jipya la Utawala la Shule ya Sekondari Mnolela, iliyopo kijiji cha Luhokwe, katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, kwenda kukagua ujenzi wa jengo la bweni la wasichana Shule ya Sekondari ya Kineng’ene, akiwa katika ziara yake hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Uwanja wa Fisi Lindi jana  Januari 21, 2012, wakati wa ziara hiyo.


 
Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi Uwanja wa Fisi Lindi jana.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili baada ya Makamu wa Rais, kumaliza kuwahutubia wananchi wa Uwanja wa Fisi, mkoani Lindi jana
.

No comments:

Post a Comment