TANGAZO


Sunday, January 22, 2012

Benki ya Posta Tanzania yasaidia Shule ya Msingi Temeke

 
Meneja wa Kitengo cha Mikopo, benki ya Posta Tanzania (TBP), Abdallah Mtandika, akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa wadau mbalimbali kuchangia elimu ya watoto wetu kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 2, kwa shule ya Msingi Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta, Noves Moses na Mwenyekiti wa Kamati ya shule Rajab Ndunda na kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Said Mbolembole. (Picha na Mdau wetu) 

 Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses (kulia), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2, ikiwa ni mchango wa Benki hiyo kuisaidia Shule ya Msingi Temeke kukabiliana na changamoto mbalimbali. Wapili ni Meneja wa Kitengo cha Mikopo benki ya Posta Abdallah Mtandika, Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Temeke, Rajab Ndunda na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Temeke Bakir Makele.
Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses (kulia), akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2, ikiwa ni mchango wa Benki hiyo, kuisaidia Shule ya Msingi Temeke kukabiliana na changamoto mbalimbali. Wapili ni Meneja wa Kitengo cha Mikopo benki ya Posta Abdallah Mtandika, Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Temeke, Rajab Ndunda na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Temeke Bakir Makele.

No comments:

Post a Comment